Baraza la usalama la umoja wa
mataifa limepiga kura kwa kauli moja kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini
kama adhabu ya kufanyia majaribio zana zake za nuklia.
Vikwazo hivyo vinalenga kuhujumu uwezo wa Pyongyang kufadhili na kutoa kawi kwa mpango wake wa nuklya.Vikwazo hivyo vilevile vinatoa masharti kwa biashara ya kununua mafuta mbali na kupiga marufuku uuzaji wa nguo katika mataifa ya kigeni.
Maamuzi hayo ya baraza la usalama la umoja wa mataifa yaliungwa mkono kwa wingi wa kura baada ya Marekani kuondoa mpango wake wa kutaka uungwaji mkono kutoka Urusi na China
Korea Kusini inasema kuwa kwa kuhujumu amani Korea Ksakzini itaewekewa vikwazo zaidi vya kimataifa.
- Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
- Malaysia yaishutumu Korea Kaskazini
- Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa
Kura hiyo ilipitishwa baada ya washirika wa Pyongyang ikiwemo Urusi na China kuilazimu Marekani kupunguza vikwazo hivyo.
Vikwazo hivyo ambavyo vilipitishwa katika baraa hilo la umoja wa mataifa vilipingwa na Korea Kaskazini.
Taarifa ya chombo cha habari cha Korea Kaskazini KNCA imeonya kwamba iwapo Marekani itasisitiza vikwazo vikali dhidi ya taifa hilo Korea Kasakzini itahakikisha kuwa Marekani inagharamikia hilo.
Hatua ya Marekani ya kutaka Korea Kaskazini kuwekewa vikwazo vya ununuzi wa mafuta kutoka nje ilionekana kama hatua itakayoliyumbisha taifa hilo.
- Trump: tutaidhibiti Korea Kaskazini
- Trump: Korea Kaskazini imeanza kutuheshimu
- Korea Kaskazini yawekewa vikwazo vipya
Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Nikki Haley aliambaia baraza la usalama la umoja wa mataifa baada ya kura hiyo kwamba hatufurahii kuiongezea vikwazo Korea kaskazini. hatutaki vita.
Msemaji wa rais wa Korea Kaskazini alisema siku ya Jumanne :Korea Kaskazini inahitaji kujua kwamba hujuma yoyote dhidi ya amani ya kimataifa itapelekea taifa hilo kuwekewa vikazo zaidi.