.

Welcome to Our Blog

LightBlog

Tuesday, 12 September 2017

Korea Kaskazini: Tutailetea Marekani machungu makubwa

Korea Kaskazini imetishia Marekani na kusema kuwa itasababisaha machungu makali ambayo Marekani haijawai kushuhudia kufuatia vikwazo vipya vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa.
Mjumbe wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa ameishutumu Marekani kwa kutafuta makabiliano ya kisiasa , kiuchumi na kijeshi.
Mapema Marekani iliapa kuweka shinikizo zaidi ikiwa Korea Kaskazini itaendela na njia zake hatari.
Vikwazo vya Umoja wa Mataifa ni hatua ya kuhakikisha kuwepo uhaba wa mafuta na kipato kufuatia mipango yake ya nyulia.
Hatua hizo zinapiga marufuku uuzaji mafuta kwenda Korea Kaskazini na uuzuaji wa bidha kutoka Korea Kaskazini baada ya jaribio la sita na kubwa zaidi la bomu la nyuklia mapema mwezi huu.
Han Tae Song, ambaye ni balozi wa Korea Kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa alisema amekataa kile alichokitaja kuwa vikwazo vilivyo kinyume na sheria.
"Hatua zitazochukuliwa na Korea Kaskazini zitaisababishia Marekani machungu makali ambayo hajawai kushuhudiwa katika historia yake," aliambia mkutano huko Geneva.