.

Welcome to Our Blog

LightBlog

Wednesday, 13 September 2017

Tetesi za soka Ulaya

Rais wa klabu ya PSG nchini Ufaransa Nasser al-Khelaifi ana matumaini makubwa kwamba klabu hiyo haijakiuka sheria za usajili za Fifa baada ya kumsajili Neymar kwa kitita cha uhamisho wa £200m kilichovunja rekodi ya dunia mbali na usajili mwengine wa Kylian Mbappe aliyeigharimnu klabu hiyo kitita cha £165m.
Rais wa PSG Al-Khelaifi pia amethibitisha kuwa vilabu vingine vilitoa kitita cha juu zaidi ya £165m watakachomlipa Mbappe.(Daily Mirror)


Arsenal itapata fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema msimu ujao kwa kuwa klabu hiyo inamsaka mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoinne Griezmann na mwenzake wa Juventus Paulo Dybala (Don Balon via Daily Star)
Dybala ametaka kujiunga na mchezaji mwenza wa Argentina Lionel Messi katika klabu ya Barcelona lakini amesisitiza kuwa anafurahia kusalia katika klabu hiyo ya Italy.(FourFourTwo)

West Ham wamekosa kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Andre Schurrle kutoka klabu ya Dortmund katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (Sun)
Real Madrid wamejiunga na Liverpool katika mbio za kumwania mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Timo Werner. (TalkSport)
Leicester wanatumaini kwamba winga Damarai Gray, 21, atatia saini kandarasi mpya ya mapato ya £50,000 kwa wiki(Daily Telegraph)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba anadai kwamba beki wa Tottenham Serge Aurier, 24, ambaye alijiunga na Spurs kutoka Paris St-Germain, amesajiliwa na klabu isiyomfaa(Daily Express)
Mkufunzi wa Trabzonspor Muharrem Usta anasema kuwa alifanya mazungumzo ya moja kwa moja na kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 25, kuhusu uhamisho wa mkopo kuelekea katika klabu hiyo ya Uturuki lakini mpango huo ukakwama katika dakika za mwisho.(Turkish-Football via Daily Star)

Barcelona imechelewesha usajili wa beki wa Palmeiras Yerry Mina ,22, ili kutomkasirisha Lionel Messi na Javier Mascherano. (Diario Gol via Daily Express)
Mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller amesema kuwa alipendelea kuelekea Manchester United miaka miwili iliopita ,na sasa mchezaji huyo ,27, amaesema kuwa kuna uwezekana mkubwa akahamia klabu hiyo siku za usoni (Manchester Evening News)
Beki wa klabu ya Sporting Kansas, Erik Palmer-Brown, 20, ametia saini kandarasi ya awali na Manchester City na atajiunga na klabu hiyo mnamo mwezi Januari (ESPN)

Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amemkosoa mshambuliaji Robert Lewandowski baada ya mchezaji huyo ,29, kuhoji kwa nini mabingwa hao wa Ujerumani hawakutumia fedha kama zile zilizotumiwa na PSG pamoja na Barcelona kununua wachezaji wapya. (Daily Mail)