Wachezaji wa Uingereza na
wafanyikazi wake watashauriwa kutotumia mtandao wa Wi-fi katika maeneo
ya uma ama hata katika hoteli wakati wa kombe la dunia la mwaka ujao
nchini Urusi kutokana na hofu ya kudukuliwa.
Shirikisho la soka
nchini Uingereza lina wasiwasi kwamba habari muhimu kama vile majeraha ,
kikosi kitakachochaguliwa pamoja na maelezo mengine ya kiufundi huenda
zikadukuliwa.Hofu ya wizi wa data pia imeangaziwa kufuatia udukuzi wa mwezi uliopita uliofanywa na kundi la Fancy Bears kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku katika soka.
Kundi hilo linadai kwamba habari hizo zilizofichuliwa mnamo mwezi Agosti zinaonyesha kwamba takriban wachezaji 160 walifeli vipimo vya utumizi wa dawa za kusisimua misuli 2015, huku idadi hiyo ikidaiwa kuongezeka na kufikia 200 mwaka uliofuta.
FIFA inasema inaendelea kuzuia mashambulizi ya kiusalama.