Wabunge kutoka chama kinachotawala
nchini Uganda NRM wamekubaliana kuwasilisha mswada ambao unapendekeza
kuondewa miaka ya kuwania urais nchini Uganda.
Ikiwa watafaulu
mswada huo utamwezesha Rais Yoweri Museveni ambaye anaaminika kuwa
mwenye umri wa miaka 73, kuwania tena uchaguzi wa mwaka 2021.Amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 na kwa sasa anahudumu muhula wake wa tano madarakani.
- Rais Museveni: Sijaugua kwa miaka 31
- Museveni amteua mwanawe kuwa mshauri
- Mwanaharakati akamatwa kwa 'kumtusi' Janet Museveni
Wengi wanasema kuwa NRM ambacho kina wabunge wengi, kitasababisha mabadiliko ya katiba lakini wengibe ndni ya NRM waekana.
Wabunge wanasema kuwa watawasilisha mswada huo bungeni katika kipindi cha wiki moja.