Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
amewataka wabunge kuheshimu katiba wakati wa kufunguliwa bunge kwenye
kikao chake cha kwanza tangu ufanyike uchaguzi wa tarehe 8 Agosti.
Rais
Kenyatta alisema kuwa kipindi hiki ambacho Kenya inasubiri kurudiwa kwa
uchaguzi uliofutwa na mahakana, ni muhumu kwa katiba kuheshimiwa.Alirejelea matamshi yake kuwa hakubaliani na uamuzi wa mahakama ya juu wa mwezi uliopitawa kufuta matokeo ya urais, lakini alikubali kwa sababu anaheshimu katiba.
Lakini Kenyatta alisema kuwa hadi pale rais mpya ataapishwa yeye bado ni rais.
- Mahakama yafutilia mbali ushindi wa Kenyatta
- Odinga: Mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa
- Uchaguzi Kenya: Upinzani washutumu serikali kwa mauaji
- Mahakama yaamrisha bunge kutekeleza sheria ya jinsia Kenya
Wakati wa kufunguliwa kwa bunge NASA nao walikuwa wakiendelea na mkutano wao katika ngome yao kisiasa, mtaa wa Kibera mjini Nairobi.
Bunge linafunguliwa huku wakenya wakijiandaa tena kupiga kura tarehe 17 mwezi Oktoba.
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya iliamrisha uchaguzi wa urais kurudiwa kutoka na hitilafu zilizotokea kwenye uchaguzi mkun uliofanyika tarehe 8 mwezi Agosti.