.

Welcome to Our Blog

LightBlog

Tuesday, 12 September 2017

Afrika Kusini yakubali kurudia mechi na Senegal

Viongozi wakuu wa Afrika Kusini wamekubali mechi wa kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2018 ambapo Afrika Kusini iliibuka mshindi inastahili kurudiwa.
Shirikisho la kandanda duniani FIFA lilitoa ilani kwamba mechi hiyo irudiwe baada ya mwamuzi wa mechi hiyo Joseph Lamptey kupigwa marufuku kwa kutoisimamia vyema mechi hiyo.
Shirikisho la kandanda wa Afrika Kusini (Safa) limekuwa likitathmini jinsi ya kukata rufaa lakini kwa sasa wamesema wamekubaliana na Fifa.
Hata hivyo shirikisho hilo limesema lingekata rufaa iwapo mashtaka ya mwamuzi huyo yngebatilishwa.
Afrika Kusini iliichapa Senegal magoli 2-1 katika mechi waliotoka sare mwaka jana.
Siku ya Jumanne Safa ilisema ''imeamua kwa misingi ya kimaadili na nidhamu kwamba mechi hii ilibatilishwe.
''Iwapo korti itabatilisha uamuzi huo, kila kitu kitakuwa hakitambuliki na Safa watakosa nafasi ya kukosoa uamuzi wa Fifa wa kurudia mechi hiyo.
''Maelezo yote ya Safa kwamba kazi zake hazihusiani na hongo, basi kwa misingi hiyo ndio tumeamua kuyafuata maagizo ya Fifa.''
Safa imekuwa ikifikiria kukata rufaa kwani ilikuwa imeshauriana na wachunguzi ambao walikuwa wakifanyia mechi hiyo uchunguzi.
Hii inamaanisha Afrika Kusini sasa wako katika nafasi ya mwisho katika kundi D na alama moja katika mechi tatu walizoshiriki na sasa Senegal wako katika nafasi ya tatu na alama nne.
Burkina Faso imeongoza katika kundi lake na alama sita , mbele ya taifa la kisiwani Cape Verde kutokana na tofauti ya goli moja, huku ikiwa na mshindi katika hatua ya makundi ndiye atakaye fuzu katika michuano ya kombe la Dunia itakayo andaliwa nchini Urusi.
Fifa itatoa uamuzi wake tarehe 14 kwa siku halisi kwa mechi hiyo ya marudiano , ambayo inatarajiwa kuchezwa katika dirisha la uhamisho wa kimataifa- mwezi mmoja kabla droo ya Kombe la Dunia mwaka 2018.
Afrika kusini wala Senegal hazijalaumiwa kwa makosa yoyote