.

Welcome to Our Blog

LightBlog

Wednesday, 13 September 2017

''Barcelona bado ipo miongoni mwa timu mbili bora duniani''

Barcelona bado ipo miongoni mwa timu mbili bora duniani licha ya kumpoteza Neymar kulingana na kocha wa Juventus Massimiliano Allegri.
Juve ambao walipoteza fainali ya msimu uliopita ya kombe la vilabu bingwa dhidi ya Real Madrid inaelekea Barca siku ya Jumanne katika mechi ya kundi D.
Mshambuliaji wa Brazil Neymar aliondoka na kuelekea PSG msimu huu baada ya uhamisho wake wa £200m uliovunja rekodi ya dunia.
''Pamoja na Real Madrid ni timu ambazo zina uwezo mkubwa wa kushinda ubingwa huo'', alisema Allegri.
''Wamempoteza Neymar na kumnunua kinda Ousmane Dembele , lakini pamoja na Real Madrid wanasalia kuwa timu mbili bora duniani''.
Juventus iliishinda Barcelona 3-0 kwa jumla msimu uliopita katika robo fainali.
Mkufunzi huyo anadhani kwamba iwapoa wataishinda Barcelona kwa mara ya tatu mfululizo itakuwa kitu muhimu sana.
''Tunajua kwamba kucheza mara tatu mfululizo dhidi ya Barcelona baada ya kucheza mara mbili mwaka uliopita bila kufungwa ni vigumu sana hata iwapo tunaweza''.
Barcelona wameshinda mechi zake zote tatu za La Liga chini ya mkufunzi mpya Ernesto Valverde.